< 以西結書 36 >

1 「人子,你向以色列群山講預言說:以色列群山,聽上主的話罷!
“Mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana.
2 吾主上主這樣說:因為敵人曾論你們說:『哈! 永遠荒涼了,那地已成了我們的產業。』
Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu adui wanasema juu yako, “Aha! Mahali palipoinuka pa zamani pamekuwa milki yetu.”’
3 為此你要預言說:吾主上主這樣說:因人使你們荒涼了,從各方面侵蝕你們,使你們成為殘餘民族的產業,並使你們成為人們的口頭禪和話柄:
Kwa hiyo tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu wamewafanya ukiwa na kuwagandamiza kila upande ili mpate kuwa milki ya mataifa mengine na kuwa kitu cha kusimangwa na kudhihakiwa miongoni mwa watu,
4 為此,以色列群山! 你們聽吾主上主的話罷! 吾主上主這樣對高山、丘陵、溪澗、山谷、荒涼的廢墟,以及那些曾為四周殘餘民族的掠物和笑柄而被遺棄的城邑說:
kwa hiyo, ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana Mwenyezi: Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka,
5 吾主上主這樣說:我必在我妒火中發言攻斥各殘餘的民族和整個厄東,她們心裏懷著幸災樂禍,和輕視的心情,將我的地方據為自己的產業,劫掠它當作戰利品。
hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’
6 為此,你向以色列地域講預言,對高山、丘陵、溪澗和山谷說:吾主上主這樣說:因為你們遭受了異民的凌辱,看,我必在妒火和憤怒中發言。
Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa.
7 為此,吾主上主這樣說:我舉手起誓:你們四周的異民必要遭受他們當受的凌辱。
Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninaapa kwa mkono wangu ulioinuliwa kwamba mataifa wanaowazunguka nao pia watadharauliwa.
8 以色列群山,你們要給我的百姓以色列生出枝葉,結出果實,因為他們快來到了。
“‘Lakini ninyi, ee milima ya Israeli, mtatoa matawi na matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa sababu hivi karibuni watakuja nyumbani.
9 看,我偕同你們,眷顧你們,使你們得以耕種,得以播種,
Mimi ninawajibika nanyi na nitawaangalia kwa upendeleo, mtalimwa na kupandwa mbegu,
10 在你們那裏增加全以色列家族的人數,使城邑再有居民,廢墟得以重建。
nami nitaizidisha idadi ya watu kwenu, naam, nyumba yote ya Israeli. Miji itakaliwa na watu na magofu yatajengwa upya.
11 我要在你們那裏,使人和牲畜的數目增多,他們要增加繁殖;我要使你們再有居民,如同昔日一樣,優待你們勝過先前,如此,你們便承認我是上主。
Nitaongeza idadi ya watu na wanyama juu yenu, nao watazaana sana na kuwa wengi mno. Nitawakalisha watu ndani yenu kama ilivyokuwa wakati uliopita, nami nitawafanya mfanikiwe kuliko hapo kwanza. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
12 我要引領人,即我的百姓以色列到你們上面,他們要佔領你,你要成為他們的產業,再不使他們喪失子女。
Nitawafanya watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watawamiliki ninyi, nanyi mtakuwa urithi wao, kamwe hamtawaondolea tena watoto wao.
13 吾主上主這樣說:因為人向你說:你吞噬了人,並使你的百姓喪失子女;
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu watu wanakuambia, “Unawala watu na kuliondolea taifa lako watoto wake,”
14 從此你不再吞噬人,也不再使你的百姓喪失子女──吾主上主的斷語──
kwa hiyo hutakula tena watu wala kulifanya tena taifa lako lisiwe na watoto, asema Bwana Mwenyezi.
15 我不再讓在你那裏聽到異民的凌辱,你也不再受異民咒罵,也不再使你的百姓喪失子女──吾主上主的斷語。」
Sitakufanya tena usikie dhihaka za mataifa, wala kudharauliwa na kabila za watu, wala kulifanya taifa lako lianguke, asema Bwana Mwenyezi.’”
16 上主的話傳給我說:「
Neno la Bwana likanijia tena, kusema:
17 人子,以色列家族住在自己的地域時,以自己的品行和作為玷污了此地,他們的品行在我面前好似經期的污穢。
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi.
18 因他們在此地所流的血,又因他們的偶像玷污了此地,我遂在他們身上發洩我的憤怒,
Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa sababu walikuwa wamemwaga damu katika nchi na kwa sababu walikuwa wameitia nchi unajisi kwa sanamu zao.
19 將他們分散在異民中,散佈在各國,照他們的品行和作為懲罰了他們。
Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakaenda huku na huko katika nchi mbalimbali, nikawahukumu sawasawa na mwenendo wao na matendo yao.
20 他們到了應去的異民那裏,還褻瀆了我的聖名,因為人們論及他們說:『這些人原是雅威的百姓,但他們卻應當離開他的地域! 』
Tena popote walipokwenda miongoni mwa mataifa walilitia unajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuwahusu, ‘Hawa ndio watu wa Bwana, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’
21 我遂憐惜我的聖名,即以色列家族在他們所到的異民中所褻瀆的聖名。
Lakini niliwahurumia kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli imelitia unajisi miongoni mwa mataifa huko walikokwenda.
22 為此,你要告訴以色列家族,吾主上主這樣說:以色列家族,我作這事並不是為了你們,而是為了我的聖名,即你們在所到的異民中所褻瀆的聖名。
“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Si kwa ajili yako, ee nyumba ya Israeli, kwamba ninafanya mambo haya, bali ni kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo mmelitia unajisi miongoni mwa mataifa mliyoyaendea.
23 我要使我的大名顯聖,即在異民中被褻瀆,即你們在他們中所褻瀆的聖名;當我在你們身上,在他們眼前顯為聖的時候,異民就要承認我是上主──吾主上主的斷語。
Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana Mwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.
24 我要把你們從異民中領出,從各地聚集你們,領你們回到你們的地域。
“‘Kwa kuwa nitawaondoa ninyi toka mataifa, nitawakusanya kutoka nchi zote na kuwarudisha kwenye nchi yenu wenyewe.
25 那時,我要在你們身上灑清水,潔淨你們,淨化你們,脫離各種不潔和各種偶像。
Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka uchafu wenu wote na kutoka sanamu zenu zote.
26 我還要賜給你們一顆新心,在你們五內放上一種新的精神,從你們的肉身內取去鐵石的心,給你們換上一顆血肉的心。
Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.
27 我要將我的神賜與你們五內,使你們遵行我的規律,恪守我的誡命,且一一實行。
Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu.
28 如此,你們要居住在我賜給你們祖先的地方;你們要作我的百姓,我作你們的天主。
Mtaishi katika nchi niliyowapa baba zenu, ninyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.
29 我要救你們脫離各種不潔,命五穀豐登,不再讓你們遭受饑荒。
Nitawaokoa ninyi kutoka unajisi wenu wote. Nitaiita nafaka na kuiongeza iwe nyingi sana nami sitaleta njaa juu yenu.
30 我要使樹上的果實,天間的出產豐收,免得你們因饑荒受異民凌辱。
Nitaongeza matunda ya miti na mazao ya mashamba, ili kwamba msipate tena aibu miongoni mwa mataifa kwa ajili ya njaa.
31 那時你們記起了你們的惡行和那些不好的行為,連你們自己對你們的罪過和醜惡之事,也感覺討厭。
Ndipo mtakapozikumbuka njia zenu za uovu na matendo yenu maovu, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya dhambi zote na matendo yenu ya kuchukiza.
32 你們應清楚知道:我作這事並不是為了你們──吾主上主的斷語──以色列家族! 對你們的品行害羞慚愧罷們!
Ninataka ninyi mjue kwamba sifanyi hili kwa ajili yenu, asema Bwana Mwenyezi. Oneni aibu na mkatahayari kwa ajili ya mwenendo wenu, ee nyumba ya Israeli!
33 吾主上主這樣說:在我潔化你們脫離各種罪過的那天,使城邑有人居住,廢墟得以重建,
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Siku ile nitakapowasafisha kutoka dhambi zenu zote, nitarudisha watu waishi katika miji yenu na magofu yatajengwa upya.
34 在過客眼中曾為荒蕪的地方,再得以耕種之時,
Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa badala ya kukaa ukiwa machoni mwa wale wote wanaopita ndani yake.
35 人們要說:那曾荒廢的地方,如今成了「伊甸」樂園;荒蕪廢棄和破壞的城邑,如今成了設防安居之地。
Watasema, “Hii nchi iliyokuwa imeachwa ukiwa sasa imekuwa kama bustani ya Edeni, miji ile iliyokuwa magofu, ukiwa na kuangamizwa, sasa imejengewa ngome na kukaliwa na watu.”
36 如此,你們四周的殘餘民族便承認,是我上主重建了破壞的城,種植了荒廢的地。我上主言出必行。
Ndipo mataifa yanayowazunguka yaliyobakia watakapojua kuwa Mimi Bwana nimejenga tena kile kilichoharibiwa na nimepanda tena kile kilichokuwa ukiwa. Mimi Bwana nimenena, nami nitalifanya.’
37 吾主上主這樣說:我還要讓以色列家族求我實行這事:叫他們的人數繁殖,多如羊群;
“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mara nyingine tena nitasikia maombi ya nyumba ya Israeli na kuwatendea jambo hili: Nitawafanya watu wake kuwa wengi kama kondoo,
38 就如被奉獻的羊群,就如在慶節日耶路撒冷的羊群有多少,荒蕪的城邑也要充滿那麼多的人群:如此,他們便承認我是上主。」
kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.”

< 以西結書 36 >